SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA MAKUZI NA MALEZI YA WATOTO

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA MAKUZI NA MALEZI YA WATOTO

Like
284
0
Thursday, 27 August 2015
Local News

SERIKALI imeahidi kuendelea kufanya jitihada mbalimbali katika kuendeleza makuzi na malezi ya watoto katika familia ili kujenga Taifa lenye watu wenye maadili.

Akifungua kongamano la wadau wa haki za watoto Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dokta Pindi Chana amesema Serikali inashughulikia marekebisho ya kisera na mipango zilizopo ili kukuza upatikanaji wa haki za watoto nchini.

 Kongamano la wadau wa malezi na makuzi ya familia limefanyika muda ambao mpango wa utekelezaji wa malengo ya milenia unafikia ukingoni, ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.

Comments are closed.