SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA ZA MABASI YAENDAYO KASI NA FLYOVER

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA ZA MABASI YAENDAYO KASI NA FLYOVER

Like
249
0
Monday, 25 May 2015
Local News

SERIKALI imeahidi kuendelea kuchukua jitihada za kutosha katika kuhakikisha inakamilisha miradi ya ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasi na za flyover ili kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi dokta JOHN MAGUFULI wakati akijibu swali la mbunge wa kinondoni mheshimiwa IDD AZZAN aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali katika kutekeleza miradi hiyo.

Waziri MAGUFULI amesema kuwa jitihada za kufanikisha miradi hiyo zinaendelea kuchukuliwa  ambapo hadi sasa kuna makampuni ambayo yameomba kusimamia ujenzi huo ikiwemo China engenereng  ya nchini humo.

 

Comments are closed.