SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUINUA UTALII WA NCHI

SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUINUA UTALII WA NCHI

Like
197
0
Monday, 06 July 2015
Local News

SERIKALI imeahidi kushirikiana vyema na sekta binafsi katika masuala ya kuinua utalii wa nchi kwa lengo la kuhakikisha Taifa linaingiza mapato ya kutosha kupitia sekta hiyo.

Hayo yamesemwa leo bungeni mjini Dodoma na naibu waziri wa maliasili na utalii mheshimiwa MAHMOUD MGIMWA wakati akijibu swali la mbunge wa Ilala mheshimiwa Mussa Zungu aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali juu ya suala hilo.

Mheshimiwa Mgimwa amesema kuwa ingawa sekta ya utalii imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi lakini serikali ipo tayari kuhakikisha inazishirikisha ipasavyo sekta binafsi ili kukabiliana na changamoto hizo pamoja na kuleta manufaa kwa wananchi.

Comments are closed.