SERIKALI YAAHIDI KUWAWEZESHA WAVUVI WADOGO

SERIKALI YAAHIDI KUWAWEZESHA WAVUVI WADOGO

Like
206
0
Friday, 29 January 2016
Local News

SERIKALI imewahakikishia wananchi hususani wavuvi wadogo kuwa itahakikisha inawawezesha wavuvi hao kufanya shughuli zao za uvuvi kwa manufaa ili kujiletea maendeleo yao pamoja na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi mheshimiwa Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Mwibara mheshimiwa Kangi Lugola aliyetaka kufahamu jitihada za serikali katika kuwanufaisha wavuvi.

Katika majibu ya swali hilo pia mheshimiwa Nchemba amewataka watu wenye dhamana ya kusimamia shughuli mbalimbali kutowanyanyasa wavuvi hususani wanawake kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sharia.

Comments are closed.