SERIKALI YAANDAA MPANGO WA KUSHIRIKISHA SHUGHURI ZA KILIMO NA VIWANDA ILI KUONGEZA THAMANI YA MAZAO

SERIKALI YAANDAA MPANGO WA KUSHIRIKISHA SHUGHURI ZA KILIMO NA VIWANDA ILI KUONGEZA THAMANI YA MAZAO

Like
275
0
Friday, 30 January 2015
Local News

KATIKA kupambana na umasikini nchini Serikali imeaandaa mpango wa kushirikisha shughuli za kilimo na viwanda ili kuongeza thamani ya mazao kwa wakulima yanayouzwa nje ya nchi badala ya kuendelea kuuza mazao ghafi kwa thamani ndogo.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Kilimo na Chakula STEVEN WASIRA alipozungumza katika Mkutano wa maswala ya Kilimo ulioandaliwa na Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa-IFAD- ambapo amesema mpango huo utawawezesha wakulima wadogo kuinuka kiuchumi na kuepukana na umasikini unaowasumbua wakulima wengi nchini.

Mheshimiwa Wasira amesema pamoja na mpango wa serikali kuzisaidia kaya masikini kwa kuzipatia fedha taslim kupitia TASAF serikali imeandaa mpango wa miaka kumi kuanzia mwakani kuinua kilimo na kuimarisha sekta ya viwanda nchini.

Comments are closed.