SERIKALI YAANDAA UTARATIBU KUWEKA MFUMO MPYA WA MAKAZI MISHANO

SERIKALI YAANDAA UTARATIBU KUWEKA MFUMO MPYA WA MAKAZI MISHANO

Like
220
0
Friday, 30 October 2015
Local News

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali inaandaa utaratibu wa namna ya kuweka mfumo mpya wa makazi kwenye eneo la Mishamo, wilayani Mpanda ili wakazi hao waondokane na hali ya kuishi kama wakimbizi.

 

Waziri Pinda ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa eneo hilo waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira Mishamo uliokuwa na lengo la kutoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa kuwapatia uraia waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972.

 

Katika hafla hiyo amebainisha kuwa Serikali ilishafanya uamuzi kwamba kila kata iwe na huduma zote muhimu ili kila mtu apate nafasi ya kuendesha shughuli zake kwa malengo.

Comments are closed.