SERIKALI YAENDELEA NA MPANGO WA KUTOA ELIMU YA MSINGI KWA WATOTO

SERIKALI YAENDELEA NA MPANGO WA KUTOA ELIMU YA MSINGI KWA WATOTO

Like
215
0
Wednesday, 17 December 2014
Local News

SERIKALI INAENENDELEA na mpango wake wa kutoa Elimu ya msingi kwa watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dokta SHUKURU Kawambwa wakati akiwasilisha mada inayohusu “Namna Tanzania inavyoboresha Usawa wa Kinga ya Jamii katika Sekta ya elimu” katika kongamano la Kimataifa linaloendelea katika siku ya pili jijini Arusha kuhusu Kinga ya Jamii.

Dokta KAWAMBWA ameeleza kuwa mpango huo umeanzia Elimu ya Awali, shule ya Msingi na Sekondari ambapo kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule apate Elimu ambayo ndiyo msingi wa kinga ya jamii nchini tofauti na awali ambapo elimu ya msingi ilikuwa kwa watoto wenye Umri kuanzia miaka 7 hadi 14.

Comments are closed.