SERIKALI imelitaka Shirikala la Umeme nchini-Tanesco kuhakikisha linafuatilia mita zenye matatizo hususani za luku, ili kuondoa usumbufu kwa wateja wao na kuwafungia mita zinazofanya kazi.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage wakati akijibu swali la mheshimiwa Diana Chilolo, Mbunge wa Viti Maalum, katika kipindi cha maswali na majibu.
Katika swali lake Mheshimiwa Chilolo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya mita mpya ambazo zinatolewa sasa na TANESCO ambazo umeme unapokuwa mdogo zinazima ikilinganishwa na zile za zamani ambazo hazina matatizo.