SERIKALI YAKAMILISHA MIPANGO YA KUVUTA MAJI SAFI NA SALAMA KUTOKA ZIWA VICTORIA

SERIKALI YAKAMILISHA MIPANGO YA KUVUTA MAJI SAFI NA SALAMA KUTOKA ZIWA VICTORIA

Like
351
0
Wednesday, 18 March 2015
Local News

SERIKALI imekamilisha Mipango ya kuvuta Maji Safi na Salama kutoka Ziwa Victoria, kwa ajili ya wakazi wa Miji ya Tabora,Nzega, na Igunga mkoani Tabora.

Pia,Serikali ya India imekubali kuipatia Tanzania Dola za Marekani Milioni 100 kwa ajili ya kuongeza Maji katika jiji la Dar es salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani,ambako kwa sasa unakamilishwa mradi mkubwa.

Katika awamu nyingine uvutaji wa Maji kutoka Ziwa Victoria,Serikali inakusudia kuanza mazungumzo na India kwa ajili ya kupatiwa

mkopo ambao utapeleka maji katika Miji ya Magu,Bariadi,Maswa,Kishapu,Shinyanga na Simiyu.

Comments are closed.