SERIKALI YAKIRI CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA AJIRA

SERIKALI YAKIRI CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA AJIRA

Like
943
0
Monday, 21 September 2015
Local News

PAMOJA na kuwepo na maendeleo ya kuridhisha katika suala la ajira kwa vijana, serikali imekiri kwamba ukosefu wa ajira bado ni tatizo kubwa kwa Taifa na duniani kwa ujumla.

 

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kazi kutoka Wizara ya kazi Ally Ahmed wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa ajira kwa vijana na kusema kuwa kutokana na changamoto hiyo kwa sasa suala la Ajira limekuwa Ajenda kuu ya Taifa.

 

Mbali na hayo amebainisha kuwa vijana wanaojiajiri wenyewe wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la mtaji ikiwemo maeneo ya kufanyia kazi na utaalamu katika ujasiriamali utakaowawezesha kuendesha miradi wanayoibuni.

A3

Mkurugenzi wa kazi wizara ya kazi na ajira, Ally Msaki Ahmed, akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Eric Shitindi katika warsha ya kitaifa ya ajira kwa vijana iliyofanyika hoteli ya Duble Tree by Hilton. Katika hotuba yake aliwataka washiriki kujadili kwa makini matatizo ya vijana na kutoa suluhu itakayosaidia watendaji kutunga sera na kutoa mwelekeo mpya wa kukabiliana na tatizo hilo.

 

 

A2

Comments are closed.