SERIKALI YAOMBWA KUBORESHA MITAALA YA ELIMU KATIKA SHULE ZA MSINGI

SERIKALI YAOMBWA KUBORESHA MITAALA YA ELIMU KATIKA SHULE ZA MSINGI

Like
303
0
Wednesday, 25 November 2015
Local News

SERIKALI imeombwa kuboresha mitaala ya Elimu katika shule za misingi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vipindi vya jinsia huku serikali ikishirikiana kikamilifu na  Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo Ukeketaji, Ndoa za Utotoni pamoja na Mimba za utotoni ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya walimu wa shule za misingi kupitia  Shirika la jukwaa la utu wa mtoto- CDF, walipokuwa wanatoa Elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kupita njia ya Filamu ya Ghati na Rhobi ambayo ilizinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga.

Comments are closed.