SERIKALI YAOMBWA KUCHUNGUZA WANAOJINUFAISHA NA HARAMBEE ZA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

SERIKALI YAOMBWA KUCHUNGUZA WANAOJINUFAISHA NA HARAMBEE ZA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

Like
215
0
Thursday, 02 July 2015
Local News

SERIKALI kupitia vyombo vya ulinzi na Usalama vimeombwa kuchunguza  Asasi, Taasisi, Mashirika na watu binafsi wanaotumia mwamvuli wa matatizo ya watu wenye ulemavu wa ngozi kujinufaisha kwa kufanya harambee mbalimbali.

Katibu wa Chama cha Maalbino Wilaya ya Temeke Gaston Mcheka ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam baada ya kile alichodai kuchoshwa na tabia ya baadhi ya watu kukusanya pesa kwa ajili ya kuwasaidia albino na badala yake kutokomea pasipo walengwa kunufaika.

Comments are closed.