SERIKALI YAOMBWA KUFANYA UKAGUZI WA MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA KIJAMII

SERIKALI YAOMBWA KUFANYA UKAGUZI WA MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA KIJAMII

Like
245
0
Wednesday, 17 February 2016
Local News

SERIKALI imeombwa kufuatilia na kukagua maeneo yaliyotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo shule, hospitali na zahanati ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Diwani wa kata ya Buguruni Adam Fugame alipokuwa akizungumza na wanahabari kwa lengo la kumuomba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik kuukabidhi uongozi wa kata kiwanja alichowahi kukikabidhi mwaka 2011 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ambacho kimekodishwa kwa kampuni ya Yasser General Supply kama eneo la kupaki magari

Fugame amesema kuwa kumekuwa na tatizo la elimu ya sekondari kwenye kata hiyo hali inayosababisha watoto zaidi ya 200 kushindwa kuendelea na masomo ya seondari kwa ukosefu wa shule ya kata.

Comments are closed.