SERIKALI YAOMBWA KUTAFUTA NJIA MBADALA KUPUNGUZA FOLENI DAR

SERIKALI YAOMBWA KUTAFUTA NJIA MBADALA KUPUNGUZA FOLENI DAR

Like
356
0
Tuesday, 07 July 2015
Local News

SERIKALI imeombwa kuona umuhimu wa kutafuta njia mbadala ya kuhakikisha inapunguza foleni katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuruhusu maeneo ya bandari kavu kutumika kama barabara kuu ya kupitishia  maroli ya mizigo.

Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Amani Mkowa wa Dar es Salaam ALPHONCE TEMBA wakati akizungumza na kituo hiki juu ya namna ya kupunguza msongamano wa magari ya mizigo yanayosababisha foleni barabarani.

Amesema kuwa maeneo kama Chalinze, Ruvu kigwaza na Mlandizi yanaweza kujengwa bandari hizo hali itakayochangia kupunguza tatizo hilo ambalo linasababisha kushuka kwa kiwango cha ukuaji wa uchumi nchini.

Comments are closed.