SERIKALI YAOMBWA KUTOA ELIMU YA URAIA KWA VIONGOZI WA KIMILA MKOA WA MANYARA

SERIKALI YAOMBWA KUTOA ELIMU YA URAIA KWA VIONGOZI WA KIMILA MKOA WA MANYARA

Like
392
0
Monday, 06 July 2015
Local News

KITUO cha Sheria na Haki za binadamu nchini –LHRC– kimeiomba Serikali kutoa elimu ya uraia katika mchakato wa katiba mpya kwa viongozi wa kimila wa mkoa wa Manyara ili waifikishe kwa jamii inayowazunguka.

Mwanasheria wa kituo hicho Lengai Merinyo ameyasema hayo wakati akizungumza na jamii ya wafugaji wa kata ya Partimbo wilayani Kiteto juu ya elimu ya uraia kwa mpiga kura kuhusu katiba pendekezwa.

Merinyo amesema ili kuwezesha jamii ya mkoa wa Manyara kunufaika na kuuelewa mchakato wa katiba mpya juhudi za dhati zinatakiwa kuchukuliwa kwa kuwaelimisha kwanza viongozi wa kimila kwani wana nguvu katika jamii yao.

 

Comments are closed.