SERIKALI YAPITISHA AZIMIO LA KINGA YA JAMII

SERIKALI YAPITISHA AZIMIO LA KINGA YA JAMII

Like
257
0
Thursday, 18 December 2014
Local News

SERIKALI ya Tanzania imepitisha Azimio linalohusu Kinga ya Jamii lenye msingi imara wa kusimamia masuala hayo nchini na Afrika kwa ujumla ili kuwa na maendeleo halisi kwa watu wake.

 

Azimio hilo limepitishwa na kusainiwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali jijini Arusha wakati wa kufunga kongamano la kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii ambalo limeshirikisha wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika.

 

Akitoa hotuba ya kufunga kongamano hilo Waziri Saada amesema kuwa maazimio yaliyofikiwa katika kongamano hilo yametoa mwelekeo na msingi wa kuimarisha kinga ya jamii kwa wananchi.

Comments are closed.