SERIKALI YASAINI MKATABA KUKUSANYA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

SERIKALI YASAINI MKATABA KUKUSANYA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

Like
229
0
Thursday, 30 July 2015
Local News

SERIKALI imesaini Mkataba wa Makubaliano ya kukusanya fedha kiasi cha shilingi Milioni 12 laki 3, elfu sitini na mbili na 969 za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini.


Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa Jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Mkuya na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania –TRA– Bernard Mchomvu kwenye hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya Fedha na mamlaka hiyo.


Mbali na kusaini mkataba huo Waziri huyo amewaasa watendaji wa TRA kuwawekea wafanyakazi mazingira mazuri ya kutekeleza wajibu wao inavyopaswa kwa mujibu wa sheri, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Comments are closed.