SERIKALI YASHAULIWA KUWEKA VIPAUMBELE UWEKEZAJI  SEKTA BINAFSI

SERIKALI YASHAULIWA KUWEKA VIPAUMBELE UWEKEZAJI SEKTA BINAFSI

Like
304
0
Tuesday, 18 November 2014
Local News

SERIKALI kupitia ofisi ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji imeshauriwa kuweka kipaumbele suala la uwekezaji katika sekta binafsi ili kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuwa sekta hiyo ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika maendeleo ya Taifa.

Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na mwenyekiti wa kamati ya uchumi ya bunge mheshimiwa LUHAGA MPINA wakati akichangia muswada wa marekebisho ya sheria baina ya sekta ya umma na sekta binafsi uliyosomwa kwa mara ya pili na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji dokta MARY NAGU kwa lengo la kuboresha usimamizi wa ubia baina ya sekta hizo.

Mbali na hayo Mheshimiwa MPINA amesema kuwa ili serikali iweze kunufaika katika masuala mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu inapaswa kuzitumia ipasavyo sekta binafsi.

 

Comments are closed.