SERIKALI imeshauriwa kuandaa Sheria ya Mirathi kwa kuzingatia na kupitia Sheria za Dini, Mila na Desturi za Watanzania badala ya kuendelea kutumia Sheria namba 36 ya mwaka 1963 ya nchini India ambayo haikidhi Mahitaji ya Watanzania.
Akizungumza na EFM Wakili wa Kampuni ya Uwakili ya MEGA PAUL KALOMO amesema kuwa Tanzania haina sheria yake ya Mirathi hali inayopelekea kuwepo na mikanganyiko katika suala la mirathi ambapo imekuwepo ya Dini na Mila ambayo inamkandamiza mwanamke.