SERIKALI YASHAURIWA KUBORESHA MISHAHARA YA WAALIMU

SERIKALI YASHAURIWA KUBORESHA MISHAHARA YA WAALIMU

Like
291
0
Wednesday, 23 September 2015
Local News

SERIKALI imeshauriwa kuboresha mishahara ya walimu ili waweze kufanya kazi kwa bidii tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa wakifanya  kazi wakiwa na mawazo yakutojua kesho yao.

Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Rais wa chama cha ngumi Tanzania MUTTA RWAKALE  wakati wa mahafali ya 12   darasa la saba  shule ya msingi UKWAMANI  ambapo amesema kuwa  kutokana na walimu kuwa na mishahara midogo   inaweza kuchangia kufeli kwa wanafunzi kutokana na kutokuwa  makini wakati wakufundisha huku wakiwaza namna ya kupata fedha  yakujitosheleza kimaisha.

Comments are closed.