SERIKALI YASHAURIWA KUBORESHA NA KUWEKEZA KATIKA MFUMO WA ELIMU NCHINI

SERIKALI YASHAURIWA KUBORESHA NA KUWEKEZA KATIKA MFUMO WA ELIMU NCHINI

Like
205
0
Monday, 01 June 2015
Local News

SERIKALI imeshauriwa kuboresha na kuhakikisha inawekeza ipasavyo katika mfumo wa elimu nchini ili kuleta matokeo bora ya elimu na kuimarisha shughuli za ushindani wa kiuchumi baina yake na nchi jirani.

Ushauri huo umetolewa leo mjini Dodoma na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamii mheshimiwa MARGARETH SITTA mara baada ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi kuwasilisha makadilio ya matumizi ya wizara hiyo.

Akichangia hoja ya makadilio kwa wizara hiyo mbunge wa kuteuliwa mheshimiwa JAMES MBATIA amesema kuwa kwa kiasi kikubwa serikali imeshindwa kuboresha sera ya elimu hali inayosababisha kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.

Comments are closed.