SERIKALI YASHAURIWA KUDHIBITI MATUMIZI YA SILAHA

SERIKALI YASHAURIWA KUDHIBITI MATUMIZI YA SILAHA

Like
228
0
Thursday, 19 March 2015
Local News

KAMBI rasmi ya Upinzani Bungeni imeishauri serikali kusimamia ipasavyo sheria ya kudhibiti matumizi ya silaha nchini ili kuimarisha usalama wa wananchi pamoja na kukomesha matukio hatarishi yanayoleta taswira mbaya kwa Taifa.

Akitoa taarifa rasmi ya kambi hiyo leo Bungeni mjini Dodoma mbunge wa Arusha Mjini mheshimiwa GODBLESS LEMA amesema kuwa ili wananchi wanufaike na sheria mbalimbali zinazopitishwa ni vyema kwa serikali kuzisimamia kwa haki na usawa pasipo kupendelea upande wowote.

Awali akiwasilisha muswada wa sheria ya kudhibiti matumizi ya silaha wa mwaka 2014 Naibu waziri wa wizara ya Mambo ya ndani mheshimiwa PEREIRA SILIMA amesema kuwa muswada huo utaisaidia kwa kiasi kikubwa  nchi kukabiliana na matukio ya kiharifu yanayojitokeza mara kwa mara katika baadhi ya maeneo kwa kuboresha usimamizi wa sheria hiyo.

 

Comments are closed.