SERIKALI YASHAURIWA KUIWEZESHA TAKUKURU

SERIKALI YASHAURIWA KUIWEZESHA TAKUKURU

Like
204
0
Monday, 18 May 2015
Local News

KAMATI ya Bunge ya katiba, sheria na Utawala bora imeishauri serikali kuiwezesha Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini-Takukuru-kwa kuipatia nyenzo imara ili kufanikisha shughuli muhimu hususani katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na mwenyekiti wa kamati hiyo JASSON RWEIKIZA wakati akitoa maoni ya kamati juu ya mapendekezo ya bajeti ya ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma, utawala bora, uhusiano na uratibu ambapo amesema kuwa uwezeshaji wa kutosha wa rasirimali katika taasisi hiyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha shughuli za udhibiti wa rushwa nchini.

 

 

Comments are closed.