SERIKALI YASHAURIWA KUTOA ELIMU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA KWA KUZINGATIA SERA YA MAZINGIRA

SERIKALI YASHAURIWA KUTOA ELIMU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA KWA KUZINGATIA SERA YA MAZINGIRA

Like
362
0
Friday, 24 July 2015
Local News

SERIKALI imeshauriwa kutoa elimu ya uhifadhi mazingira kwa kuzingatia sera ya mazingira kwa wananchi wanaoishi katika mkoa wa Lindi na Mtwara ambayo itasaidia kuongeza uwekezaji katika mikoa hiyo.

Akizungumza na Kituo hiki leo Afisa msimamizi kutoka baraza la taifa la hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC Muhandisi JAMES NGELEJA amesema kuwa kutokana na kugundulika kwa gesi katika mikoa hiyo hali hiyo  itachangia kuongeza kiwango cha uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii.

Amebainisha kuwa mbali na kutoa elimu ya utunzaji na uhifadhi mazingira lakini pia  Serikali inawajibu wa kuandaa semina mbalimbali zitakazo lenga kutoa mafunzo ya mazingira katika vyanzo vyote vya maeendeleo na maeneo ya kihistoria.

Comments are closed.