SERIKALI YASHAURIWA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA MAHAKAMA

SERIKALI YASHAURIWA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA MAHAKAMA

Like
246
0
Thursday, 21 May 2015
Local News

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya katiba, sheria na utawala bora imeishauri serikali kuwajengea uwezo watumishi wa mahakama pamoja na kuwapatia mahitaji yote muhimu ikiwemo vitendea kazi bora ili kufanikisha utendaji wao wa kazi.

Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Bukoba mheshimwa JASSON RWEIKIZA ambapo amesema kuwa uwekezaji wa kutosha katika sekta hiyo ya mahakama ni muhimu kwa kuwa ni miongoni mwa chombo maalumu cha kuleta haki na usawa kwa wananchi.

Comments are closed.