SERIKALI YASHAURIWA KUWEKA MIKAKATI KUSAIDIA KUTOA MAFUNZO IMARA KWA WANANCHI

SERIKALI YASHAURIWA KUWEKA MIKAKATI KUSAIDIA KUTOA MAFUNZO IMARA KWA WANANCHI

Like
243
0
Wednesday, 18 March 2015
Local News

SERIKALI imeshauriwa kuweka mikakati imara itakayosaidia utoaji wa mafunzo maalumu kwa wananchi hususani katika sekta ya gesi ili kuondokana na uhaba wa wataalam wa gesi nchini.

Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na mbunge wa jimbo la Lushoto mheshimiwa HENRY SHEKIFU wakati akichangia muswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za wageni ya mwaka 2014 uliowasilishwa na waziri wa kazi na Ajira mheshimiwa GAUDENCIA KABAKA.

Mheshimiwa SHEKIFU amesena kuwa utoaji wa mafunzo hayo kwa watanzania utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa wataalam wa masuala ya gesi na kupunguza gharama zinazotolewa na serikali katika kuwalipa wataalam kutoka nje ya nchi.

 

Comments are closed.