SERIKALI YASHAURIWA KUWEKA MIKAKATI YA KUANZISHWA KWA MFUKO WA KUJITEGEMEA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

SERIKALI YASHAURIWA KUWEKA MIKAKATI YA KUANZISHWA KWA MFUKO WA KUJITEGEMEA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

Like
233
0
Tuesday, 03 February 2015
Local News

SERIKALI imeshauriwa kuweka mikakati bora itakayowezesha kuanzishwa kwa mfuko wa kujitegemea kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na kuboresha tume ya kupambana na kudhibiti Ukimwi –TACAIDS- ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo na kuliletea Taifa maendeleo.

 

Akitoa taarifa za utekelezaji wa kamati ya masuala ya Ukimwi leo Bungeni mjini Dodoma mwenyekiti wa Kamati hiyo LEDIANA MNG’ONG’O amesema kuwa endapo mfuko huo utaanzishwa utaisaidia nchi kwa kiasi kikubwa katika kupambana na ugonjwa huo pasipo kutegemea msaada kutoka nchi jirani.

 

Kwa upande wake mheshimiwa DIANA CHILOLO mjumbe wa kamati hiyo amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa maambukizi ya ukimwi yanapungua ni vyema pia serikali ikadhibiti matumizi ya dawa za kulevya kwani ni njia mojawapo ya kuchochea maambukizi hayo.

Comments are closed.