SERIKALI YASHAURIWA KUWEKA MUDA RASMI WA KUFANYA UCHUNGUZI WA MAKOSA MBALIMBALI

SERIKALI YASHAURIWA KUWEKA MUDA RASMI WA KUFANYA UCHUNGUZI WA MAKOSA MBALIMBALI

Like
259
0
Friday, 03 July 2015
Local News

WABUNGE wameishauri serikali kuweka muda rasmi wa kufanya uchunguzi wa makosa mbalimbali ili kuokoa ucheleweshwaji wa kutoa hukumu kwa watuhumiwa kulingana na makosa.

Akichangia maoni yake leo bungeni mjini Dodoma mbunge wa Singida Mashariki mheshimiwa TUNDU LISSU amesema kuwa ni muhimu kwa serikali kuweka kipengele hicho ili kutatua changamoto za ucheleweshwaji wa kesi kutokana na uchunguzi mbovu.

Naye mbunge wa ubungo mheshimiwa JOHN MNYIKA amewataka wabunge wa chama tawala kutotumia wingi wao katika kupitisha hoja bila kusikiliza upande wa upinzani.

Comments are closed.