SERIKALI YASISITIZA KUTENDA HAKI KWA VIONGOZI WANAORUHUSIWA KUJIHUSISHA NA SIASA

SERIKALI YASISITIZA KUTENDA HAKI KWA VIONGOZI WANAORUHUSIWA KUJIHUSISHA NA SIASA

Like
226
0
Wednesday, 27 January 2016
Local News

SERIKALI imesisitiza kuwa ipo makini kuhakikisha kuwa kila kiongozi anayeruhusiwa kujihusisha na masuala ya kisiasa anapata haki yake bila usumbufu wowote.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa nchi Ofisi ya rais, Utumishi na Utawala bora Mheshimiwa Angela Kairuki wakati akijibu swali la mheshimiwa Hafidhi Ali Tahir Mbunge aliyetaka kufahamu utaratibu wa serikali juu ya watumishi hao.

Mheshimiwa Kairuki amesema kuwa watumishi ambao hawaruhusiwi kujihusisha na masuala ya kisiasa ni pamoja na Wanajeshi wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, Jeshi la polisi na vyombo vingine vya Ulinzi na usalama.

Comments are closed.