SERIKALI nchini imetakiwa kuzingatia kasi ya ongezeko la idadi ya watu katika mipango yake ya maendeleo ikiwemo uwekaji wa mikakati bora na uboreshaji wa sera ili kuweka uwiano sahihi kati ya ongezeko la watu na maendeleo ya Taifa.
Hayo yamebainishwa jana Jijini Dar es salaam na wajumbe na mabalozi wa kikundi kazi kinachoundwa na wadau na watetezi wa masuala ya uzazi wa mpango na idadi ya watu-TCDAA– ambapo kwa upande wa mwakilisi mwandamizi wa kikundi kazi hicho Bi. Halima Shariff amesema imefika wakati kwa serikali kujipanga na kuendena na kasi hiyo kwa kutengeneza nafasi za ajira ili kukabiliana na ukuaji huo.