SERIKALI YATANGAZA WANAFUNZI WATAKAOJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2015

SERIKALI YATANGAZA WANAFUNZI WATAKAOJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2015

Like
430
0
Thursday, 18 December 2014
Local News

WANAFUNZI 438,960 kati ya 451,392 waliofaulu katika mtihani wa darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015 katika shule za sekondari za serikali Nchini.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa upande wa elimu KASSIM MAJALIWA alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.28 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.8 ikilinganishwa na mwaka jana ambao ilikuwa ni asilimia 96.3.

Mheshimiwa MAJALIWA amesema wanafunzi wengine waliobakia watachaguliwa kujiunga na shule hizo katika uchaguzi wa awamu ya pili unaotarajiwa kufanyika mwezi wa pili mwakani 2015, baada ya kukamilisha zoezi la ujenzi wa madarasa unaoendelea sasa.

Akizungumzia udanganyifu katika mitihani Mheshimiwa Majaliwa amesema kiwango kimepunguwa kutoka wanafunzi 13 mwaka 2013 hadi kufikia wanafunzi 4 kwa mwaka huu wa 2014.

 

Comments are closed.