SERIKALI YATARAJIA KUFUNGUA MAABARA YA MADINI

SERIKALI YATARAJIA KUFUNGUA MAABARA YA MADINI

Like
244
0
Thursday, 13 August 2015
Local News

TANZANIA inatarajia kufungua maabara ya madini itakayo kuwa ikitumiwa na Nchi zote zinanzozunguka ukanda wa Maziwa makuu kwa ajili ya kuchunguza madini kwa kutumia teknolojia ya alama ya vidole, kutambua madini yanapotokea ili kudhibiti utoroshwaji wake na baishara haramu katika nchi hizo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Injinia Ngosi Mwihava katika Mkutano wa Kongamano la nchi za Maziwa makuu-ICGLR wenye lengo la kujadili namna ya kutumia alama za vidole kubaini asili ya madini-AFP.

Comments are closed.