SERIKALI YATOA TAMKO JUU YA ADHA YA MAJI DAR

SERIKALI YATOA TAMKO JUU YA ADHA YA MAJI DAR

Like
253
0
Tuesday, 31 March 2015
Local News

SERIKALI imetoa tamko kuhusu utekelezaji wa upatikanaji wa huduma ya Maji safi na uondoaji wa maji taka katika jiji la Dar es salaam ili kupunguza adha na matatizo wanayoyapata wakazi wa jiji ambao idadi yake inaongezeka kila siku.

Akizungumza wakati wa kutoa hoja hiyo  Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Maji Profesa JUMANNE MAGHEMBE amesema Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kuona ukubwa wa Tatizo hilo jijini,kufatia hoja binafsi juu ya tatizo hilo iliyowahi kutolewa na Mbunge wa Jimbo la Ubungo JOHN MNYIKA ambapo imeonekana mahitaji ya maji ni Lita Milioni Mia Nne Hamsini kwa siku katika jiji la Dar es salaam.

 

Comments are closed.