SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI TAARIFA YA URUSHAJI WA MATANGAZO YA BUNGE

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI TAARIFA YA URUSHAJI WA MATANGAZO YA BUNGE

Like
262
0
Thursday, 28 January 2016
Local News

SERIKALI imetolea ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji kwa umma kuwa imefuta vipindi vya shughuli za Bunge kuoneshwa katika televisheni ya Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) zilizoenea katika maeneo mbalimbali.

 

Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye wakati akizungumza na wananchi moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini kutolea ufafanuzi taarifa hizo.

 

Mheshimiwa Nape amesema Serikali haijafuta vipindi vya Bunge bali ilichofanya ni kubadilisha muda wa kurusha vipindi hivyo kutoka muda wa mchana na kuviweka usiku kwa lengo la kupunguza gharama za kurusha moja kwa moja matangazo hayo.

Comments are closed.