SERIKALI YAWASILISHA BUNGENI MUSWADA WA MAAFA KWA MARA YA PILI

SERIKALI YAWASILISHA BUNGENI MUSWADA WA MAAFA KWA MARA YA PILI

Like
193
0
Friday, 20 March 2015
Local News

SERIKALI imewasilisha Bungeni kwa mara ya pili Muswada wa Sheria ya usimamizi wa maafa ya mwaka 2014 itakayokuwa na malengo ya kuboresha na kuondoa mapungufu katika sheria iliyopo kwa manufaa ya Taifa.

Akiwasilisha rasmi Muswada huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu ,Mheshimiwa JENISTER MHAGAMA amesema kuwa, sheria inayopendekezwa katika muswada huo itasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha uratibu na kutatua matatizo ya maafa katika eneo husika.

Mheshimiwa MHAGAMA amebainisha kuwa kumekuwepo na mapungufu mengi katika sheria ya maafa iliyopo hali inayosababisha madhara makubwa wakati wa maafa hivyo ni muhimu maboresho yakafanyika ili kuondokana na tatizo hilo.

Comments are closed.