SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA 78 NIGERIA

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA 78 NIGERIA

Like
408
0
Wednesday, 26 November 2014
Global News

WATU 78 wameuawa katika mashambulio mawili ya kujitoa mhanga yaliyofanywa sokoni, katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema mlipuko wa kwanza ulitokea wakati washambuliaji hao walipomuwekea mlipuko mwanamke mmoja mwenye matatizo ya akili.

Kundi la kiislamu la wapiganaji la Boko Haram ambalo linadhibiti maeneo mengine ya miji ya kaskazini mwa nchi hiyo na vijiji, linadhaniwa kuhusika na shambulio hilo.

Comments are closed.