SHAMBULIO LEBANON: TISA WAKAMATWA

SHAMBULIO LEBANON: TISA WAKAMATWA

Like
189
0
Monday, 16 November 2015
Global News

IDARA za Usalama nchini Lebanon zimefanikiwa kuwakamata watu Tisa wanaodhaniwa kuhusika katika shambulio lililotokea Alhamisi ya wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.

Taarifa zinaeleza kwamba watu Saba kati ya tisa wanaoshikiliwa na Polisi ni raia wa Syria huku wengine wawili ni raia wa Lebanon huku tayari kundi la wapiganaji wa Kiislamu limedai kuhusika na shambulio hilo.

Hata hivyo Wachunguzi wamebaini kuwa washambuliaji hao waliilenga hospitali inayoendeshwa na taasisi ya wapiganaji wa majeshi ya Kilebanon ya madhehebu ya Shia, Hezbollah.

Comments are closed.