Shambulizi la Skripal: Marekani kuiwekea vikwazo Urusi, kuanzia Agosti

Shambulizi la Skripal: Marekani kuiwekea vikwazo Urusi, kuanzia Agosti

Like
431
0
Thursday, 09 August 2018
Global News

Marekani imepanga kuweka vikwazo vipya kwa Urusi ikiwa ni kujibu kitendo
cha shambulizi la sumu la afisa wa zamani wa usalama wa Urusi Sergei Skripal
na mtoto wake wa kike nchini Uingereza.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Heather Nauert, amesema
nchi yake imegundua kuwa Urusi ilitumia kemikali hatari kumshambulia
Skripal na binti yake wa kike jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria za
kimataifa.
Hii ni mara ya tatu Marekani inaiwekea vikwazo nchi fulani kwa kukiuka
sheria hii.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatano , wizara ya mambo ya nje ya Marekani
ilithibitisha kuchukua hatua dhidi ya Urusi kuhusiana na tukio la uvamizi kwa
kutumia sumu ya kemikali kwa Sergei Skripa na binti yake lililofanyika nchini
Uingereza.
Msemaji wa wizara hiyo Heather Nauert amesema imegundulika kuwa Urusi
ilitumia sumu hiyo kinyume cha sheria za kimataifa.
Serikali ya Uingereza imeopongeza hatua hiyo kwa kusema ilistahili kwa nchi
ambayo inatabia zisizo za kiungwana na ambazo hazivumuliki.
Vikwazo hivyo vipya vinatarajia kuanza Agosti 22 vikigusia zaidi uzuiaji wa
vifaa vya umeme na teknolojia nyingine kwenda na kutoka Urusi.
Marekani inasema vikwazo vingine vingi zaii vinatarajia kufuata iwapo Urusi
itashindwa kuuthibitishia ulimwengu kuwa itaacha mara moja matumizi ya
kemikali za aina hiyo.
Hii ni mara ya tatu Marekani kuweka vikwazo kwa nchi iliyotumia kemikali
katika mashambulizi dhidi ya binaadam, ikifanya hivyo kwa Syria na Korea
Kaskazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *