SHAMBULIZI LAUA WATU 60 NIGERIA

SHAMBULIZI LAUA WATU 60 NIGERIA

Like
200
0
Wednesday, 19 August 2015
Global News

RIPOTI kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa karibu watu 60 huenda waliuawa wakati wa shambulizi katika kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo lililoendeshwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa na Boko Haram.

Shambulizi hilo lilitokea katika jimbo la Yobe lilifanyika Alhamisi iliyopita na habari hizo zimepatikana kutoka kwa wale walionusurika.

Walioshuhudia wamesema kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliwasili katika kijiji hicho wakitumia pikipiki ambapo walianza kuwafyatulia watu risasi.

Comments are closed.