BARAZA kuu la Waislamu Tanzania-BAKWATA, linafanya Mkutano Mkuu leo mjini Dodoma huku ajenda kuu ikiwa ni kumchagua mfti mkuu wa Tanzania.
Mufti atakayechaguliwa atakuwa ni wa awamu ya tatu, baada ya kutanguliwa na Mufti Hemed Bin Jumaa bin Hemed na Mufti Issa Bin Simba aliyefariki dunia Juni 15 mwaka huu.
Hivi sasa nafasi hiyo inakaimiwa na Shekh Abubakari Zubery ambaye pia ameingia katika miongoni mwa wanaowania nafasi hiyo ambayo ni ya juu katika Baraza hilo akichuana na Ally Muhidin Mkoyogole, Hamis Abas Mtupa na Hassan Ibrahim Kiburwa.