SHEIKH PONDA AACHIWA HURU

SHEIKH PONDA AACHIWA HURU

Like
209
0
Monday, 30 November 2015
Local News

BAADA ya kukaa zaidi ya miaka miwili mahabusu hatimaye mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa morogoro leo imemwachia huru katibu wa taasisi na jumuiya za kiislamu Tanzania Shekhe Ponda Issa Ponda baada ya kuonekana hana hatia kwa makosa yaliyokuwa yakimkabili.

 

Hukumu hiyo imesomwa na hakimu wa mahakama hiyo bi Mary Moyo amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa pande zote mbili yaani upande wa mashitaka na upande wa mshitakiwa mahakama imemuona mtuhumiwa hana hatia na kumwachia huru kutokana na kifungu namba 235 kifungu kidogo cha kwanza cha mwenendo wa mashauri ya jinai sura ya ishirini marejeo ya mwaka elfu mbili na mbili.

Comments are closed.