SHEIN AAPISHWA ZANZIBAR LEO

SHEIN AAPISHWA ZANZIBAR LEO

Like
320
0
Thursday, 24 March 2016
Local News

RAIS Mteule wa Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein anaapishwa leo kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar.

Kuapishwa kwa Dk Shein kunamfanya apate nafasi nyingine ya kuongoza Zanzibar kwa muda wa miaka mitano ijayo, baada ya mgombea huyo wa CCM kushinda urais wa Jumapili kwa kujinyakulia asilimia 91 ya kura zilizopigwa.

Serikali pia imetangaza kuwa leo pia ni siku ya mapumziko visiwani humo ili kuwapa nafasi wananchi wahudhurie sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wao. Wageni ambao wanatarajia kuhudhuria kwenye sherehe hizo ambazo zimeanza saa 2 asubuhi ni Rais John Magufuli na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa kitaifa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Comments are closed.