SHEPOLOPOLO KUTUA DAR LEO TAYARI KUMENYANA NA TWIGA STARS

SHEPOLOPOLO KUTUA DAR LEO TAYARI KUMENYANA NA TWIGA STARS

Like
314
0
Wednesday, 08 April 2015
Slider

Timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Zambia (Shepolopolo) inatarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano kati yake na kikosi cha Twiga stars katika mchezo wa kugombania nafasi ya kushiriki michuano ya Afrika mwaka huu inayotarajiwa kufanyika Congo Brazzaville kuanzia Septemba 4-9.

Kwenye mchezo huo kikosi cha Twiga stars chini ya kocha Rogasian Kaijage iwapo kitashinda kitakuwa kimefuzu kwenda kwenye fainali hizo kufuatia matokeo ya awali ambapo waliibuka na ushindi wa magoli  4-2 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Nkoloma jijini Lusaka nchini Zambia

Mechi hiyo ya marudiano itachezwa siku ya Ijumaa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Wazambia hao watapata nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja huo kabla ya mechi ili kuuzoea na kujiweka fiti mara ya mwisho kabla ya mechi.

Comments are closed.