Nchini Rwanda sheria mpya ya makosa ya jinai imeanza kutumika.
Miongoni mwa makosa hayo ni kosa la kudhalilisha viongozi wa serikali kwa kutumia maandishi au kuchora vibonzo.
Mchoraji atahukumiwa kifungo cha hadi miaka miwili gerezani na faini ya dola takriban elfu moja na mia tano.
Kosa la kudhalilisha rais wa nchi hiyo mhusika atahukumiwa hadi miaka 7 gerezani na faini isiyopungua dola elfu 8.
Waandishi wa habari wameingiwa na wasi wasi.