SHIRIKA LA NDEGE LA EMIRATES KUWAAJIRI WATANZANIA

SHIRIKA LA NDEGE LA EMIRATES KUWAAJIRI WATANZANIA

Like
428
0
Thursday, 22 January 2015
Local News

KATIKA  kutekeleza moja ya malengo ya Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kupitia Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Nchini Dubai katika Falme za Kiarabu, umefanikiwa  kulishawishi Shirika la Ndege la Emirates  kuajiri Watanzania  kwenye Shirika hilo.

Shirika Limekubali kuajiri Watanzania katika kada mbalimbali, ambapo Maafisa wanaosimamia ajira kutoka Dubai wanatarajiwa kuja nchini Mwezi Machi mwaka huu kwa ajili ya kufanya usaili kwa Watanzania watakaoomba kazi kwenye Shirika hilo na kupata uteuzi wa awali.

Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Simba Yahaya ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam, alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ambapo amefafanua kuwa kupitia wandishi hao, Watanzania wenye sifa wataweza kufahamishwa juu ya fulsa za ajira katika Shirika hilo na kutuma maombi ya kazi.

 

Comments are closed.