SHIRIKA LA NDEGE LA UJERUMANI LATOA TANGAZO KUFUATIA KUANGUKA KWA NDEGE YAKE

SHIRIKA LA NDEGE LA UJERUMANI LATOA TANGAZO KUFUATIA KUANGUKA KWA NDEGE YAKE

Like
236
0
Wednesday, 01 April 2015
Global News

SHIRIKA la ndege la Ujerumani, Lufthansa limetoa tangazo kuhusu taarifa lilizokuwa nazo juu ya matatizo ya kiakili ya Andreas Lubitz, rubani msaidizi wa ndege ya Germanwings iliyopata ajali ambaye anadhaniwa kuiangusha ndege hiyo kwa makusudi, na kuuwa watu wote 150 waliokuwemo.

Shirika hilo limesema kwamba Lubitz, mwaka 2009 aliiarifu shule ya marubani ya shirika hilo, kwamba siku za nyuma alikuwa na matatizo makubwa ya msongo wa mawazo.

Tangu kutokea kwa ajali hiyo Jumanne wiki iliyopita, taarifa nyingi zimekuwa zikijitokeza kuhusu matatizo ya kiakili ya rubani huyo.

 

Comments are closed.