SHIRIKA LA THE FOUNDATION FOR TOMORROW LAZINDUA KAMPENI KUSAIDIA ELIMU YA WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU

SHIRIKA LA THE FOUNDATION FOR TOMORROW LAZINDUA KAMPENI KUSAIDIA ELIMU YA WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU

Like
207
0
Friday, 17 July 2015
Local News

SHIRIKA lisilo la kiserikali la The Foundation for Tomorrow limezindua kampeni ya kuchangia SHAMIRI ya kusaidia elimu ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu lengo ni kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 50 zitakazowawezesha kupata elimu bora na kuondokana na mazingira yanayowakabili.

 

Meneja Mahusiano wa shirika hilo Anton Asukile ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni maalumu ya SHAMIRI inayolenga kusaidia ustawi wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

 

Asukile ameiomba jamii ya Watanzania kushiriki katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii ili kuwakomboa watoto hao kwa kuchangia kampeni ya SHAMIRI.

Comments are closed.