SHIRIKISHO LA RIADHA KENYA YALAUMIWA

SHIRIKISHO LA RIADHA KENYA YALAUMIWA

Like
253
0
Friday, 28 August 2015
Slider

Wakili aliyeongoza jopo lililochunguza sakata ya utumizi wa dawa zilizoharamishwa michezo nchini Kenya, Moni Wekesa, amesema kuwa shirikisho la mchezo wa riadha nchini Kenya, AK limeshindwa kukabiliana na janga hilo.

Wekesa amesema kwamba tukio la kukamatwa na hatimaye kupigwa marufuku kwa wanariadha wawili wa Kenya mjini Beijing ni tukio la aibu na linaiharibia Kenya sifa.

Hata hivyo amesema tangu matokeo ya jopo lake kutolewa, Kenya imepiga hatua kukabiliana na janga hilo ila wakuu wa michezo nchini humo wamezembea.

Ameitaka serikali kuwashurutisha wanariadha hao Koki Manunga na Joyce Zakary kuelezea walipewa na nani dawa hizo zilizopigwa marufuku.

Aliyekuwa mwanariadha maarufu nchini Kenya, Mike Boit naye amesema tukio hilo limeiharibia wanariadha wa Kenya sifa, kwani huenda wanariadha wasiotumia dawa hizo wakalengwa na kushukiwa kuwa walaghahi.

Mapema mwaka huu mwanariadha maarufu Rita Cheptoo pia alipatikana na hatia ya kutumia dawa hizo na kwa sasa anatumikia adhabu ya kutoshiriki kwa mashindano yoyote ya riadha kwa miaka miwili.

Katika kipindi cha miwiki miwili iliyopita zaidi ya wanariadha wa Kenya 30 wamepatikana na hatia ya kutumia dawa hizo za kusisimua misuli.

Comments are closed.