SHULE 6 ZA SEKONDARI KUJENGWA KINONDONI

SHULE 6 ZA SEKONDARI KUJENGWA KINONDONI

Like
303
0
Thursday, 31 December 2015
Local News

KUFUATIA Manispaa ya  kinondoni kukabiliwa na tatizo la upumgufu wa shule za sekondari lililosababishwa na ongezeko kubwa la wanafunzi  wanao faulu, Manispaa hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu imepanga kujenga shule sita ili kusaidia kupunguza sehemu ya tatizo hilo.

Mkuu wa wilaya ya kinondoni PAUL MAKONDA amesema ni aibu kubwa kwa manispaa kubwa kama ya hiyo kuwa na upungufu wa shule za sekondari kutokana na manispaa hiyo kuwa na wadau wengi wenye uwezo wa kusaidia kuondoa tatizo hilo.

MAKONDA ameongeza kuwa ujenzi wa shule hizo utahusisha zaidi ya kata sita na unatarajiwa kuchukua zaidi ya miezi mitatu kukamilika.

 

Comments are closed.