SHULE ZAANZA KUFUNGWA LEO KENYA

SHULE ZAANZA KUFUNGWA LEO KENYA

Like
408
0
Monday, 21 September 2015
Global News

Wakati shule zote za umma na binafsi zikianza kufungwa kuanzia leo nchini Kenya, Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta akihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa serikali ya nchi hiyo haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai walimu.

Rais Kenyatta ametoa wito mgogoro huo kutatuliwa kwa amani ingawa tayari Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu ukiendelea.

Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.

Comments are closed.